Tuesday, April 19, 2011
HERI SANA KWA SIKUKU YA PASAKA, NA SHEREHE ZA KUONGOKA KWA MT. AGUSTINO
Wapendwa wanafamilia ya Kiagustino, napenda kuchukua fursa hii kuwasalimuni nyote. Ni matuini yangu kuwa wote tunaendela kwa moyo mmoja na Roho moja tukidunda katika maisha na kila mmoja katika nafasi yake.
Nawashukuru sana wote walioweza tembelea "Lugono" (blog) yetu yawanafamilia wakiagustino. Mawazo yenu, nasaha zenu pendevu imekuwa mchango mkubwa katika harakati na juhudi zetu za kuikusanaya familia ya kiagustino pamoja. Kwani chimbuko na asili yetu ni moja (ubungu?), na dhani ni zaidi ya hilo pia... hasa "kutokukata tamaa bali kukata matuma" tukiongozwa na ule wimbo wetu wa Kiagustinooo kuishiiiiiiii aleluuuyaaaaa, kuishi kama ndugu, aleluuuyaa... hizo zote ni alama za muagustino halisi... Hatuna budi basi kulidumisha hilo na kuiendeleza roho ya kiagustino. Kila mmoja wetu anamchango wake katika harakati za kulikusanya kundi hili chini ya mchungaji mmoja.. tena wawe na umoja kama sisi tulivyo... na pia watu watatutambua kuwa niwaagustino tukiishi kwa umoja katika upendo.
Yote hiyo inawezekana tukifuata njia ya mwasisi wetu: "uongofu".
Basi tukiwa tunasherehekea sikukuu ya kuongoka kwa Baba yetu Mt. Agustino, tumwombe ili atusaidie nasi ili uongofu wetu ulenge kuwa na moyo mmoja, nia moja tukiijenga familia ya kiagustino.
NAWATAKIENI NYOTE HERI SANA KWA SIKUKUU YA PASAKA NA SHEREHE ZA KUONGOKA KWA MT. AGUSTINO.
Nolasco Msemwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment