Saturday, March 19, 2011
SALAMU KUTOKA KWA SYLVESTER JOTA
Ndugu Waagustino, ninamini tunapendana sana kwa sababu sote tulipitia pale Mahanje. Mitaa ya Ikulu Kipela, Nyota na Ngoro sote tunakujua. Ninaomba tuwe kitu kimoja kwa sababu kuyafuata mafundisho ya Mt. Augustino siyo lazima uwe padre au sista. Walei na Wakreli sote tunawajibu ule ule wa kuishi Kiagustino. Ninachelea kupata wazo la kuijali sana sikukuu ya Mt Augustino tar 28 Agosti kila mwaka kwa kukutana na kusheherekea pamoja kule Mahanje. Si vibaya kujitoa kwa siku moja kwa kila mlei au mkreli kukutana Mahanje na kusali pamoja, kuimba pamoja, kula pamoja, kucheza pamoja, na kuimba zaburi kwa pamaja kama tulivyokuwa mabungu. Huko ndiko kuishi Kiagustino na tunaweza pia kupanga mipango mingi ya kimaendeleo ya kiroho na kimwili kwa faida ya familia nzima ya Waugustino Tanzania ambao tumetapakaa kila kona ya nchi. "Un Cor Unum et Spiritus Unum"
Sylvester Jotta (Mwagustino halisi)
Chuo Mtakatifu Augustino cha Tanzania-Mwanza.
Sylvester Jotta (Mwagustino halisi)
Chuo Mtakatifu Augustino cha Tanzania-Mwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment