TUPO PAMOJA NJIANI KWA MUNGU, HATUMWACHI MTU NJIANI

Tunaomba samahani kwa kutopakia maoni yenu mapema. Kwa kweli maoni mengine yalichelewa kutokana na kutokuwa na mawasiliano mazuri kati ya mhariri aliyeko Hispania na yule wa Tanzania. Sasa hivi kila kitu kipo katika hali nzuri. Mnaombwa kutoa maoni, kutuma picha za huko mliko ili sote tulioishi pamoja tujue tupo wapi. Anwani yetu ya barua-pepe ni ileile kama inavyoonekana hapo juu.

Asanteni.

Tupo pamoja njia kuelekea kwa Mungu.

Saturday, March 19, 2011

SALAAMU KUTOKA KWA FRT. EUSEBIUS MICHAEL

Napenda kuwasalimu Waagustino wenzangu popote pale mlipo lakini zaidi wale wote

mliopitia SEKIHA au HARESE basi naomba tukumbukane zaidi kwa anwani yangu
ya baruapepe (email). Nawakumbuka sana ndugu zangu ingawa tupo mbali lakini mara nyingi nawakumbuka sana pindi nikumbukapo mambo fulanifulani ya pale Hanga, katika

Shirika lenu la Mahanje ni shirika pekee ambalo nilikuwa na marafiki wengi
ingawa wengine hawajaendelea na maisha hayo lakini nina mawasiliano nao karibu
wote basi nyie mliobaki shirikani tuendelee kukumbukana katika sala, na tuwasiliane katika mtandano. Napenda kuwapa hongera wale waliofikia daraja la upadre kama ndugu yangu Padre Msemwa ambaye tupo naye karibu huku Ulaya, pia Baba Paroko Kasase (bwana wagonjwa wetu) Padre Mfalanyombo (bwana ulinzi wetu) na ndugu yangu Padre Seraphim (mzee wa magamu) pia nampa pongezi Shemasi wetu Benard naye namkumbuka kwa kitu kimoja alikuwa na uwezo wa kula makande sahani 2 hahahahahah, naomba mniambie kama ndugu wengine kama Casto Fusi, Ambrosi Mallya, Matengelele na Oswadi bado wanafuata njia hii?

Napenda kuwakaribisha ktk ushemasi wangu
utakao fanyika hapa Ufaransa tarehe 26/3/2011 karibuni sana.Asanteni sana,

Mengi katika Kristu

Frt Eusebius Michael


1 comment:

  1. My brother suggested I might like this blog. He was entirely right.
    This post actually made my day. You cann't imagine just how much time I had spent for this information! Thanks!

    Feel free to visit my homepage :: hip waist ratio

    ReplyDelete