Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Familia ya Waagustino nchini Tanzania ni mkusanyiko wa watu wote popote walipo waliopitia katika Shirika la Mtakatifu Augustino ambao hivi sasa ni mapadre, mabradha, na walei. Familia hii inalenga kuwaleta pamoja na kuhuisha umoja wa familia ili wale wafahamiane. Tufahamishane kuhusu taarifa za Mahanje, Morogoro, Dar es Salaam na Mwanza na mahali pengine ambapo Waagustino wapo. Tuma taarifa kwa waagustinotz@gmail.com.
Tunaomba samahani kwa kutopakia maoni yenu mapema. Kwa kweli maoni mengine yalichelewa kutokana na kutokuwa na mawasiliano mazuri kati ya mhariri aliyeko Hispania na yule wa Tanzania. Sasa hivi kila kitu kipo katika hali nzuri. Mnaombwa kutoa maoni, kutuma picha za huko mliko ili sote tulioishi pamoja tujue tupo wapi. Anwani yetu ya barua-pepe ni ileile kama inavyoonekana hapo juu.
Asanteni.
Tupo pamoja njia kuelekea kwa Mungu.
Tunashukuru sana ndugu zetu waagustino kwa kuwa wabunifu na kuanzisha blogsport hii. Nawapongeza sana. Ndugu yenu Airenus Mlowe ex Augustinian
ReplyDeleteHongereni Mapadre Wapya Nolasco MSEMWA na Alois MATANDA.Mungu aambatane nanyi.Sisi waamini tuwaombee.
ReplyDeleteNdugu Waagustino. Naamini tunapendana sana kwa sababu wote tulipita pale Mahanje. Ikulu Kipela, Nyota na Ngoro wote tunakujua. Ninaomba tuwe kitu kimoja kwa sababu kuyafuata mafundisho ya Mt Augustino siyo lazima uwe padre au sista. Walei na Wakreli wote tunawajibu ule ule wa kuishi Kiagustino. Ninachelea kupata wazo la kuijali sana sikukuu ya Mt Augustino tar 28 Agosti kila mwaka kwa kukutana na kusheherekea pamoja kule Mahanje. Si vibaya kujitoa kwa siku moja kwa kila mlei au mkreli kukutana Mahanje na kusali pamoja, kuimba pamoja, kula pamoja, kucheza pamoja, na kuimba zaburi kwa pamaja kama tulivyokuwa mabungu. Huko ndiko kuishi Kiagustino na kwayo tunaweza pia kupanga mipango mingi ya kimaendeleo ya kiroho na kimwili kwa faida ya familia nzima ya Waugustino Tanzania ambao tumetapakaa kila kona ya nchi.
ReplyDelete"Un Cor Unum et Spiritus Unum"
Sylvester Jotta (Muagustino halisi)
St Augustine University-Mwanza
Ni furaha kubwa sana kuona waagustino tunaendelea vizuri tena kwa nguvu sana. Kanuni ya mt. Augustino inahimiza hasa kuishi pamoja kwa umoja. Naomba jumuiya zetu ziishi kadiri ya karama hii. Nawapongeza wataalamu wetu wanaoweza kuanzisha mitandao hii. Inatusaidia sana kulitambua shirika tena kuleta umoja kwa wale waliowahi kuishi maisha ya kiagustino. Mimi ni muagustino niliyeishi Mahanje kama mbungu mwaka 1981. Nikapata upadre Mahanje 1996. Nilipita kipindi kigumu sana katika upadre wangu. Nilifanya utume katika parokia za Mahanje, Mavurunza na Mkolani. Nikaishi katika mahangaiko kwa muda wa miaka minne katika parokia za Mbezi Beach na Makuburi kama paroko nikiwa chini ya Jimbo kuu la Dsm. Ukweli ni kwamba ndani yangu nilibaki muagustino. Mimi kama mzee nawaalika wote tuliopita Mahanje tukae katika umoja na ikiwezekana tuandae siku moja walau tualikane tukafanye sikukuu kubwa pale Mahanje na kukumbuka jinsi tulivyopita mahali pale na Mahanje ilivyotuandaa tukawa kama tulivyo. Kwa sasa nafanya utume wangu katika nchi ya PerĂº, Amerika ya kusini. Fr. Faustin J. Mlelwa OSA
ReplyDelete